Idara Ya Afya Ya Watoto

Idara hii inashughulika na Watoto chini ya miaka 14. Idara hii imeundwa kwa Vitengo viwili:

1. Watoto Wachanga chini ya siku 28

2. Watoto zaidi ya siku 28 hadi siku 14

KITENGO CHA WATOTO CHINI YA SIKU 28

Kitengo hiki kinahudumia zaidi Watoto Njiti,wenye maambukizi ya magonjwa mbalimbali na watoto wachanga wenye shida za upasuaji .

KITENGO CHA WATOTO ZAIDI YA SIKU 28

Kitengo hiki,kinahudumia watoto wenye magonjwa ya kuambukiza,magonjwa yasiyo ya kuambukiza na watoto wenye shida za upasuaji.

Idara hii ina Madaktari bingwa Wawili na Madaktari wa Kawaida Wawili. Lakini pia idara hii inapokea wanafunzi wa Utabibu kutoka chuo jirani (Sumbawanga Cotc)

pamoja na madaktari waliokatika Mafunzo kwa Vitendo ambao huzunguka idara kwa muda wa miezi mitatu.

Idara ina jumla ya Wauguzi 13 wa kada mbalimbali pamoja na mhudumu wa afya mmoja.

Mbali na Wagonjwa wa Kulazwa,idara hii pia inahudumia wagonjwa wa Nje(OPD) katika Kliniki ambayo huendeshwa mara mbili kwa wiki( Jumatatu na Ijumaa) kuanzia saa tatu Asubuhi mpaka saa Tisa na Nusu Alasiri.

Huduma za wagonjwa wa Ndani(IPD) zinapatikana Saa 24 kila siku.