MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KURAHISHA MATIBU KWA WANANCHI.

Posted on: February 8th, 2024

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Grace Maghembe amefanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga amewapongeza Wahudumu wa Hospitali kwa kutoa huduma bora kwa wananchi wa Mkoa wa Rukwa kwa kutumia mfumo wa teknolojia ya mawasiliano (Telemedicine) kwa kutuma picha kwenda kwa Mabingwa wa Radiolojia katika Hospitali ya Kanda Mbeya.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo na kukagua huduma ya Radiolojia ya CT-Scan amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa katika vifaa tiba vya kidigitali katika Sekta ya Afya ili kuboresha na kurahisisha huduma kwa jamii ngazi ya chini.

Amesema mashine hizi za kidigitali zinasaidia kurahisisha huduma, kutuma na kupokea taarifa za mgonjwa na kusaidia Hospitali ambazo hazina wataalamu kwa kushusha utaalamu huo katika hospitali husika kwa njia ya mtandao.

" Nimetembelea na kukagua huduma ya CT-Scan kwa kuangalia katika mfumo tangu ilipofungwa tarehe tisa Januari mwaka 2023 mpaka Leo wagonjwa 96 wamepata huduma".

Tarehe tisa mwezi Januari 2023 machine ya CT- Scan ilisimikwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga na mapaka sasa wagonjwa takribani 96 wamepata huduma.