WAGONJWA 392 WAMETIBIWA KATIKA KAMBI YA MADAKTARI BIGWA SRRH.

Posted on: February 9th, 2024

Takribani wagonjwa 392 wametibiwa katika kambi rasmi ya Madaktari Bingwa wa Tiba na Upasuaji wa Magonjwa ya Mifupa na Mfumo wa Mkojo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga.

Kambi hiyo iliyoanza tarehe 5 Februari hadi Leo tarehe 9 Februari imefanikiwa kutibu wagonjwa 281 wa mifupa kati ya hao kumi na tano wamefanyiwa upasuaji na kwa upande wa mfumo wa mkojo wametibiwa wagonjwa 101 kati yao watano wamefanyiwa Upasuaji.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kambi hiyo mratibu wa zoezi Dkt Joakim Michael Kisaka amesema Uongozi wa Hospitali ya Kanda Mbeya wakishirikiana na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga wamesogeza huduma hiyo ya madaktari Bingwa (huduma mkoba) kwa wakazi wa mkoa wa Rukwa kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma za kibingwa za Tiba na Upasuaji wa mifupa na mfumo wa mkojo.

Ameongeza kuwa huduma hizo ni endelevu na wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wanaendelea vizuri.