All Clinics
Kliniki za Afya ya Kinywa na meno na Kliniki za macho huendeshwa kila siku kuanzia Jumatatu
hadi Ijumaa kuanzia saa 3.00asubuhi hadi saa 9.30 mchana. Kliniki za mfumo wa Pua, Koo na
Masikio pia huendeshwa kama ilivyo kwa kliniki za meno na macho.
Hospitali inao Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya akina mama na watoto wanaoendesha Kliniki
kwa siku za Jumanne na Alhamisi kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 9.30 mchana
Hii ni kliniki ya Watoto ambayo huendeshwa mara mbili kwa wiki( Jumatatu na Ijumaa) kuanzia saa tatu Asubuhi mpaka saa Tisa na Nusu Alasiri.
Kliniki hii hutolewa na Madaktari bingwa wa Watoto.
Kliniki za upasuaji wa kawaida (General Surgery) na Upasuaji wa Mifupa (Orthopaedic Surgery)
huendeshwa kwa pamoja siku ya Jumatano kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 9.30 mchana
Kliniki ya idara hii hufanyika siku za Jumatatu na Ijumaa kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 9.30
mchana. Kliniki ni maalum kwa magonjwa ya Kisukari, shinikizo la Damu (Hypertensio), matatizo
ya figo na moyo, magonjwa ya kuambukiza, saratani, matatiz...
Kliniki za Tiba shufwaa kupitia sehemu ya Fiziotherapia huendeshwa kila siku za kazi kuanzia saa 3.00
asubuhi hadi saa 9.30 mchana
Kliniki hizi huendeshwa kwa masaa 24 kwa siku kwa mgonjwa kuwasiliana na Daktari anayemuhitaji na kulipia gharama iliyowekwa kwa huduma husika.
Hospitali pia huendesha Kliniki y Tiba na Matunzo kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI kwa siku
za Jumatatu hadi Jumamosi kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 9.30 mchana. Sehemu ya CTC pia
hutoa huduma za kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kut...
Huduma za Uchunguzi wa Saratani ya shingo ya Kizazi, Tiba ya magonjwa ya ngono na huduma za uzazi wa mpango hutolewa kwa siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi