MADAKTARI BINGWA 60 WA MAGONJWA MBALIMBALI WA DKT SAMIA KUWEKA KAMBI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA MAWENI - KIGOMA
Posted on: May 6th, 2024MADAKTARI BINGWA 60 WA DKT SAMIA KUWAHUDUMIA WAKAZI WA KIGOMA NA MIKOA JIRANI
Wakazi wa Kigoma na mikoa jirani wameombwa kujitokeze kwa wingi kwa ajili ya uchunguzi na matibabu katika Kambi maalumu ya Madaktari Bingwa wa Dkt Samia inayoendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni - Kigoma.
Akizungumza katika ufunguzi wa Kambi hiyo ya Kanda ya Magharibi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe.Salum Kali amesema madaktari hao 60 wameletwa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuwasaidia wananchi hao kuwaondolea changamoto za kiafya.
"Chakula cha Madaktari Bingwa ni magonjwa hivyo wananchi mtumie fursa hiyo kuwajulisha wengine kujitokeze kwa wingi kwa ajili ya matibabu hayo" Mhe Kali.
Mhe Kali ameongeza kuwa kupitia kambi hiyo itawasaidia kufanya utafiti wa magonjwa yanayowasumbua wakazi wa Kigoma na kufanya ufumbuzi.
Kambi ya Madaktari Bingwa wa kanda ya Magharibi iliyoanza Leo 6 Mei hadi 10 Mei imehusisha Hospitali za Rufaa za mikoa ya Sumbawanga, Kitete, Katavi na Maweni.