MAFUNZO YA TIBA MTANDAO

Posted on: August 18th, 2023

Leo wataalamu wa afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga wamepata elimu ya tiba mtandao (Tele Medicine) kutoka kwa wataalamu wa tehama kutoka Dar es salaam Institute of Technology (DIT).

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo Mkuu wa idara ya Tehama wa DIT Ombeni Mzavaamesema wamefanikiwa kufanya mafunzo hayo kwa vitendo kwa madaktari na wataalamu wa tehama katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga kwa kutuma Picha za CT scan kwenda Hospitali ya Kanda Mbeya na kupata majibu kwa haraka kutoka kwa daktari bingwa.


Ombeni amesema mradi huo uliofadhiliwa na Serikali ya Tanzania unalenga kusaidia wananchi kupata huduma za kibingwa kwa urahisi na haraka kwani taarifa za mgonjwa zitatumwa katika hospitali kubwa za Rufaa za Kikanda na za kibingwa na kujibiwa kwa haraka kupitia mfumo huo wa tiba mtandao hivyo kuokoa pesa za usafiri na muda .