MKUU WA MKOA WA RUKWA AMEKABIDHI MAGARI MAWILI SRRH YA HUDUMA ZA AFYA NA USIMAMIZI.

Posted on: February 14th, 2024

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Leo tarehe 14 Februari 2024 amekabidhi magari mawili ya huduma za Afya na Usimamizi kwa Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Akikabidhi magari hayo Mkuu wa mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere amewataka madereva kuzingatia taratibu za matumizi na kuyatunza magari hayo.

Katika kuendelea kuboresha huduma za Afya, Mkoa wa Rukwa ulipokea jumla ya Magari 10 ikiwemo magari ya wagonjwa sita na Magari ya usimamizi, ambapo hospitali ya Rufaa ya Mkoa ilipata mgawo wa Magari mawili (gari la wagonjwa na gari la Usimamizi).