TIMU YA WATAALAMU KUTOKA WIZARA YA AFYA KUKAGUA JENGO LA DAMU SALAMA NA NICU

Posted on: September 22nd, 2023


Timu ya wataalam wa Wizara ya Afya leo tarehe 22 Septemba 2023 imefanya zoezi la Conditional Survey katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga wakiongozwa na mwenyeji wao Mganga mfawidhi wa Hospitali Dkt Ismail Macha kukagua jengo la Damu Salama na kutafiti eneo kwa ajili ya Ujenzi wa wodi ya watoto wachanga njiti (NICU) ikiwa ni takwa la mkataba kabla ya kuanza utekelezaji wa afua mbalimbali za mradi ikiwemo ujenzi wa wodi za watoto wachanga na Maabara ya kuvuna damu Salama zilizochaguliwa.

Katika kuimarisha utoaji huduma muhimu za afya hususani katika eneo la afya ya mama na mtoto Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Afya Zanzibar inatekeleza programu ya uwekezaji kwenye afya ya mama na mtoto ijulikanayo kama " Tanzania Maternal and Child Investment Program" ( TMCHIP) inayofadhiliwa na Benki ya Dunia.