ZIARA YA MGANGA MKUU WA SERIKALI

Posted on: September 15th, 2023

Leo tarehe 15 Septemba 2023 Mganga Mkuu wa Serikali Prof Tumaini Joseph Nagu amefanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga kukagua huduma zinazotolewa pamoja na miundombinu ya Hospitali na kuzungumza na wananchi waliokuwa wanapata matibabu pamoja na watumishi wa Afya.

Akizungumza na watumishi wa Afya mara baada ya kufanya ukaguzi sehemu mbalimbali ndani ya Hospitali hii amewataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuzingatia usafi wakati wa kutoa huduma ili kuzuia maambukizi endapo kukitokea magonjwa ya mripuko.

Prof. Tumaini Nagu ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga kwa mazingira mazuri na huduma nzuri ya maabara na kuwataka kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amewataka kufanya usahihi wa vipimo na matibabu ili kutoa dawa sahihi kwa wagonjwa haswa dawa za Antibiotiki.