Huduma Ya Uzazi na Kujifungua
Posted on: April 10th, 2025Hospitali inatoa huduma za uzazi na kujifungua. Huduma hizi hutolewa kila siku na madaktari bingwa wa magonjwa ya uzazi na akina mama. Wananchi wanashauliwa kufuata utaratibu wa rufaa kabla ya kuja kutibiwa Hospitali Ya Mkoa. Pia tunapenda kuihimiza jamii hasa wakinamama wajawazito kuhudhuria kliniki katika vituo vya afya vilivyo jirani nao. Mama mjamzito unasisitizwa kujifungulia hospitali.